top of page

YANGA SC WAPIGWA FAINI TSH MILIONI 5 SIMBA SC MILIONI 1

Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu inaeleza kuwa

"Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) na klabu ya Young Africans ikitozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kupitia milango isiyo rasmi kuelekea mchezo tajwa hapo juu.

Baada ya kuwasili uwanjani, timu hizo hazikutumia mlango rasmi kuingia vyumbani ambapo



klabu ya Yanga imetenda kosa hilo katika michezo zaidi ya minne (4) inayozikutanisha klabu hizo za mkoani Dar es Salaam, ndani ya misimu mitatu ya 2021/2022, 2022/2023 na 2023/2024 ya Ligi Kuu.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:21 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Baada ya timu hizo kufika ndani, klabu ya Yanga haikuingia kwenye chumba maalum cha kuvalia badala yake walitumia eneo la wazi kwa ajili ya maandalizi yao kwa maelezo kuwa chumba hicho kilikuwa na harufu isiyo ya kawaida.

Klabu ya Simba ilitumia chumba maalum cha kuvalia kabla ya kuanza mchezo lakini hawakurejea kutumia chumba hicho wakati wa mapumziko.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi inasubiri taarifa ya Daktari wa mchezo huo ambaye alichukua sampuli ya hewa kutoka vyumba hivyo viwili kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page