top of page

LAWI ALIYEMVUTA JEZI AZIZ KI AFUTIWA KADI NYEKUNDU..


Taarifa kutoka Bodi ya Ligi Kuu inaeleza kuwa

"Mechi Namba 192: Young Africans SC 1-0 Coastal Union FC

Mchezaji Lameck Lawi wa klabu ya Coastal Union amefutiwa adhabu ya kadi nyekundu



aliyoonyeshwa na mwamuzi wa mchezo tajwa hapo juu baada ya kuthibitika kuwa mwamuzi huyo wa kati pamoja na mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo huo walishindwa kutafsiri vema Sheria za Mpira wa Miguu katika tukio la mchezaji huyo kumvuta jezi mchezaji Ki Aziz wa klabu ya Yanga.

Kamati ilipokea taarifa za uchambuzi wa kitaalam kutoka kwa wakufunzi wa waamuzi, ambazo zimeainisha kuwa mchezaji huyo hakustahili kuonywa kwa kadi nyekundu badala yake ilipaswa aonywe kwa kadi ya manjano kwasababu wakati tukio linatokea, kulikuwa na mlinzi mwingine wa Coastal Union mbele yake ambaye angeweza kuufikia mpira.

Uamuzi huu ni kwa kuzingatia Kanuni ya 12:8 ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi."

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page