Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya
Hii haiwezi kuwa bahati mbaya ndani ya msimu mmoja wachezaji wawili wa timu tofauti wanapewa kadi za uongo dhidi ya timu moja
Tena katika Mazingira ya kufanana pale ambapo mechi inapokua ngumu dhidi yao
Zabona Mayombwa wa Prisons alipewa kadi nyekundu ya Uongo dhidi ya Nyuma Mwiko, katika mchezo huo matokeo yalikua 2-1 na Zabona alikua tishio dhidi ya wapinzani na angeweza kabisa kuisaidai timu yake kupata ushindi au sare lakini kwa makusudi akapewa

kadi nyekundu ili kuidhoofisha Prisons
Lameck Lawi wa Coastal kapewa kadi nyekundu ya magumashi dhidi ya timu ile ile na tena katika mazingira yale yale, Mechi ilikua 0-0 na Lawi aliwadhibiti vilivyo Nyuma Mwiko, Lakini kwa makusudi akaoneshwa kadi nyekundu ili kuidhoofisha Coastal Union
Hii haiwezi kuwa bahati hata kidogo
Bodi ya ligi Tanzania mnafanya kazi nzuri sana kuzifuta hizi kadi za dhulma lakini isiiishie hapo kwani timu zinaathirika
Chunguzeni zaidi kujua kuna nini nyuma ya pazia kuzifuta kadi tuu haiwezi kuwa tiba ya kudumu ya hii dhulma
Msimu wa juzi kulikua na trend ya kutolewa Penati za uongo kumbuka Penati ya Namungo dhidi ya Nyuma Mwiko pale Ilulu Lindi
Kumbuka Penati ya Ruvu Shooting dhidi ya Nyuma Mwiko pale Kirumba Mwanza
Asante ni kwamba Waamuzi wote waliadhibiwa japo tayari timu zimeathirika
Hofu yangu ni kuwa inawezekana wamekuja style mpya ya kudhulumu kwa kutumia kadi nyekundu ndio maana naomba
Bodi ya ligi ku deal na hii kitu kwa undani ili kukomesha dhulma hii." Ahmed Ally
Comments