top of page

     MSASA MEDIA COMPANY LIMITED

 

Msasa Media Company Limited ni kampuni inayojishughulisha na masuala ya upashaji wa habari kwa njia ya kidigitali kupitia mitandao ya kijamii ( Facebook, Instagram, Twitter na Youtube)  pia tovuti ya msasaonline.co pamoja na Radio ya mtandao. Msasa Online imejikita katika ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia kwa kutoa habari, michezo, burudani na elimu kwa wafuasi wake na jamii inayozungumza lugha adimu ya Kiswahili duniani kote.. Kuwa chombo namba moja cha upashaji habari kwa njia ya kidigitali Afrika Mashariki na Kati pamoja na jamii yote inayozungumza lugha ya Kiswahili duniani kote. Pia kufungua milango ya fursa mbalimbali katika jamii ya Afrika Mashariki kupitia njia ya kidigitali.

Lengo Kuu

Kuhamasisha jamii iweze kuendana na wakati wa mabadiriko ya sayansi na teknolojia ili kupunguza msongo wa mawazo na kuelimika kwa njia ya upashanaji habari kupitia waandishi makini na wenye weredi wa hali ya juu wana hakikisha utoaji wa maudhui bora na yaliyo haririwa vyema katika saa 24 za

wiki. Malengo mbalimbali kwa ujumla. Kwa sehemu kubwa Msasa Media imelenga kundi la vijana

kama sehemu kubwa ya watazamaji wetu hivyo tunajikita katika kutoa maudhui yanayokubalika kwao huku ndani yake yakiwa ni yenye uhamasisho wenye kufungua milango ya fursa kwao hivyo kipaumbele kikubwa kinaanza kwa vijana, wanawake na pia hata kundi la watu wa makamo na wazee.

 

Malengo mengineyo ni

 

Kwa sehemu kubwa Msasa Media imelenga kundi la vijana kama sehemu kubwa ya watazamaji wetu hivyo tunajikita katika kutoa maudhui yanayokubalika kwao huku ndani yake yakiwa ni yenye uhamasisho wenye kufungua milango ya fursa kwao hivyo kipaumbele kikubwa kinaanza kwa vijana, wanawake na pia hata kundi la watu wa makamo na wazee.

 

VIPENGELE VILIVYOPO NDANI YA MSASA ONLINE

 

1. Entertainment Hub - Hii inahusisha stori/habari za mastaa kutoka Duniani kote hasa wakiwa wamefanya mambo mbalimbali makubwa ya kimaendeleo n.k

2. Msasa Trending - Hizi ni stori/habari zinazokuwa zinakiki maeneo mbalimbali iwe za Burudani, michezo, siasa , teknolojia n.k ili mradi inatrend katika wakati husika kupitia vyomba mbalimbali vya habari au mtandaoni n.k

3.Msasa Updates - Huu Ni upashaji habari tu haijarishi ina trend au lah ilimradi mna habarisha walaji juu ya jambo lolote lile liwe kubwa au dogo.

4. MsasaNews - Hizi ni habari kubwa za kitaifa na kimataifa.

5. MsasaGossipCode - Hizi ni stori zote za udaku ambazo zinapekenyua maisha ya nyota mbalimbali ili kupata umbeya n.k ikiwemo skendo mbalimbali za mastaa n.k

6. MsasaBreakTime - Hii Ni sehemu ya mapumziko inakuwa na vitu vyepesi vyepesi kama challenges au chemsha Bongo watu wanaulizwa maswali au wakati mwingine inawekwa stori za utani au za maajabu ya dunia.

6. MsasaSports - Hapa ni habari zote za michezo.

7. Msasa Love Potion - Hizi Ni story za mahusiano zenye ushauri ndani yake zinafanyika pale ambapo nyota fulani kapost qoute fulani ya mahusiano kisha tunazama ndani kuichambua maana yake pia na ushauri mbalimbali wa kimapenzi kutoka kwa wataalamu mf. Wanasaikolojia n.k

8. Msasa New Music Hapa Ni kuwajuza wadau wetu juu ya nyimbo mpya

9. Msasa Sunday Service Kila jumapili hii ni sehemu ya mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu.

10. Msasa Leo Jikoni - Mafunzo juu ya mapishi ya aina mbalimbali.

11. MsasaTech – Habari mbalimbali zinazohusu uvumbuzi wa kisayansi na Teknolojia mbalimbali.

12. Birthday Vibe – Ni sehemu ya kuwapongeza nyota mbalimbali waliozaliwa katika siku husika.

13. Msasa Fashion Killer hili ni jukwaa la mitindo mbalimbali .

14. Msasa Unusual – Hizo ni story zisizo za kawaida kutokea kwenye jamii.

15 Jicho la Mbali – Huu ni uchambuzi wa kina juu ya suala furani inakuwa makala maalumu.

16. Picha ya Nyota – Picha kali za nyota mbalimbali kama amepakia kwenye mtandao wake na ujumbe tunapita nao

KANUNI NA MUONGOZO

 

Dawati la Uhariri Msasa Online linazingatia haya.

 

1. Kuripoti habari za kweli zilizo haririwa kwa umakini.

2. Kurekebisha taarifa zilizopotoshwa ili kuwahabarisha watazamaji wetu.

3. Kuzingatia maadili ya habari kwa kuhakikisha uwiano na kutoa habari zisizo pendelea upande mmoja.

4.Kujiepusha na utoaji habari zenye udini, ukabila na yoyote yanayoweza kusababisha taharuki.

5. Kufanya kazi kwa nidhamu na weredi.

Muongozo kwa watazamaji wetu

1. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni.

2. Msasa Online inaweza kufuta maoni ambayo yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani au kusababisha taharuki.

3. Msasa Online inaweza kuzuia mtu asiweze kuona au kuweka maoni kwenye taarifa tunazohabarisha endapo atakiuka taratibu za muongozo huu.

4. Lugha chafu na zisizo na maadili haziruhusiwi.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page