Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu ya Azam FC wametoa taarifa hii ya usajili wa mchezaji mpya.
"Tumefikia makubaliano na klabu ya Stade Malien (Mali) ya kumsajili kiungo mshambuliaji wao,

Franck Tiesse.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast, amesaini mkataba wa miaka miwili atakaoanza kuutumikia kuanzia msimu ujao 2024/25.
Tiesse anayesifika kwa uwezo wake mkubwa wa kushambulia kwa kasi na uwezo wa kutumia miguu yote miwili, akiwa Stade Malien aliisaidia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Welcome to Azam FC, Tiesse!"
Comments