top of page

AZIZ KI MCHEZAJI BORA GAMONDI KOCHA BORA APRILI...

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Ki Aziz ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Aprili wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2023/2024, huku Miguel Gamondi wa Yanga akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Ki amewashinda Kipre Junior wa klabu ya Azam na Joseph Guede wa Yanga alioingia nao fainali kwenye mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Kwa mwezi Aprili, Ki alionesha kiwango kikubwa na kuwa msaada kwa timu yake katika ushindi wa michezo mitatu kati ya minne ambayo timu hiyo ilicheza, hivyo Yanga kukusanya



alama 10 na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Yanga iliifunga Singida FG mabao 3-0, ikaifunga Simba mabao 2-1, ikaifunga Coastal Union bao 1-0 kisha ikatoka 0-0 na JKT Tanzania. Ki alicheza jumla ya dakika 359 za michezo hiyo.

Kwa upande wa Gamondi aliiongoza Yanga kukusanya alama 10 katika michezo minne iliyocheza, ikishinda mitatu na sare moja, hivyo kuendelea. kuongoza ligi hiyo yenye timu 16. Gamondi amewashinda Bruno Ferry wa Azam na Malale Hamsini wa JKT Tanzania alioingia nao fainali.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam, Amir Juma kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Aprili kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page