top of page

WATU SITA WANAODAIWA KUTOA MIKOPO YA KAUSHA DAMU WAKAMATWA SONGWE..


Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania, linawashikilia Watuhumiwa 6 wanaodaiwa kufanya biashara ya huduma za Mikopo maarufu kama 'Kausha Damu' bila kuwa na Leseni


Taarifa imesema, Jeshi la Polisi liliendesha msako na kukusanya ushahidi uliosaidia kuwakamata Watuhumiwa wakiwemo Wamiliki wa Kampuni zinazotoa huduma hizo kinyume na Sheria Namba 10 ya Mwaka 2018, Kifungu cha 16

Aidha, Jeshi linawashikilia Watuhumiwa 424 waliobainika kujihusisha na matukio ya Ukatili wa Kijinsia, Wizi, Mauaji, Utapeli kwa Njia ya Mtandao, Kujifanya Mtumishi wa Umma, Kughushi Nyaraka, Dawa za Kulevya na Ukiukwaji wa Sheria za Barabarani

Watuhumiwa wengine 6 ni wanaodaiwa kughushi nyaraka zikiwemo za Kusitisha Mikataba ya Ajira, Mihuri ya Taasisi Binafsi na Serikali na Fomu za Kuchukulia Mafao ya NSSF. Wote wamefikishwa Mahakamani na Mashauri yao yapo katika hatua mbalimbali.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page