top of page

Kutoka kwa Mwigizaji Irene Uwoya amefunguka haya baada ya kutoa msaada cherehani na sehemu ya mabinti kujifunzia masuala ya urembo

Safari yangu ya kumtumikia MUNGU ilianza kama masihara siku chache zijazo ntawaeleza kwa urefu ila mwaka jana nilipata ujumbe kutoka kwa MUNGU niende Mbeya kuna watoto nikawasaidie kiukweli sikuelewa niliona labda nachanganyikiwa haikuwa rahisi nilifika Mbeya na MUNGU alinisaidia nilikutana nao kwa njia ambayo mimi mwenyewe sikutegemea Nilikuwa naona nina matatizo lakini nilipokutana nao nilijiona tajiri sana na nilimshukuru MUNGU na kumuomba msamaha mahali ambapo niliwahi kulalamika wale watoto walinifanya nilishindwa kufanya chochote nilikosa amani moyoni kwa muda mrefu sana nilimuuliza MUNGU nawezaje kuwasaidia hao watoto na hali yangu unaijua haki nilipata tabu sana nikaamua kukaaa kimya maana sikua naweza kufanya chochote wakati huo lakini kwanzia hapo nikipata pesa nasikia


sauti ikiniambia nenda Mbeya kwa wale watoto uwasaidie lakini nikawa na dharau MUNGU alinipa mtihani ambao sitokaaa nisahau ntakuja kueleza wakati mwingine ila baada ya hapo niliamua kufanya maamuzi kwenda Mbeya wale watoto walivyoniona hawakuamini walilia sana nakuniambia walikuwa wananiombea toka mwaka jana na walikuwa wakinisubiri kwa matumaini makubwa sana sababu waliamini maneno yangu nililia sanaaa nikamshukuru MUNGU walinambia wanatamani kujua kushona wengine walisema urembo nikasema ntawezaje na kiukweli sikuwa na huo uwezo wa kufanya hivyo ila nilipo tia nia tu MUNGU alifanya njia ambayo mimi mwenyewe sijawahi kuwaza ndipo nilipojua kuna wakati unapata pesa ila sio żako ni MUNGU tu anazipitisha kwako kwa ajili ya wengine basi nikafanikisha kwa kidogo MUNGU alichonijalia mimi pamoja na walioniamini wakaja na mimi kwa upendo wao mkubwa na kujitolea kwa ajili ya MUNGU na watoto hao MUNGU wa mbinguni asiwapungukie milele ndugu zangu wa @friendsofgodministry1 nawashukuru sana pia viongozi wangu wa dini zote mbili bila kujali mim ni nani au nikoje mlinipokea kwa upendo mkubwa na kuamini maono yangu

MUNGU awabariki sana pia viongozi wangu wa serikali

kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa pamoja na wilaya kwa kuweza

Kusimama na mimi kwa kila hatua.

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page