Na VENANCE JOHN
Walinzi wa pwani wa Uhispania wamesema, zaidi ya wahamiaji 230 wameokolewa kutoka kitika mashua moja siku ya jana Jumapili kwenye bahari karibu na Visiwa vya Kanari vya Uhispania. Waokoaji wamesema wanawake 14 na watoto watatu wamepatikana katika boti hiyo ambayo ilikuwa na jumla ya watu 231.

Walinzi wa pwani wa Uhispania wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya watu kuokolewa kutoka kwa boti moja nje ya kisiwa cha Gran Canaria mwaka huu. Walinzi wa pwani wa Uhispania walivuta mashua ya mbao walipowapata wahamiaji hao karibu na bandari kuu ya Gran Canaria.
Mwaka huu wahamiaji 32,878 wamechukua njia hatari kwa boti kutoka Afrika Magharibi hadi Visiwa vya Canary kati ya mwezi Januari mpaka Oktoba 15, kulingana na takwimu za serikali, ikiwa ongezeko la 39.7% kutoka kipindi kama hicho mwaka jana.
Comments