top of page

WCB WATOA UFAFANUZI KUHUSU

WCB WATOA UFAFANUZI KUHUSU

MLINZI WA DIAMOND KUDAIWA

KUMSHAMBULIA MWANDISHI

Kutoka kwenye uongozi wa lebo ya muziki ya Wasafi (WCB) inayomilikiwa na msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz wametoa taarifa hii

UFAFANUZI WA TUHUMA ZA SHAMBULIZI

Menejimenti ya Lebo ya WCB Wasafi inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma juu ya taarifa zinazosambazwa kuhusiana na mlinzi binafsi wa Msanii Nasibu Abdul Juma Issaack almaarufu kama Diamond Platnumz. Mlinzi wa msanii anahusishwa na kumshambulia mwandishi wa


Bongo Star Media TV baada ya Tamasha Usiku wa tarehe 24/02/2024 kisiwani Zanzibar.

Menejimenti inapenda kuujulisha umma ya kuwa taarifa hizo sio za kweli na zenye miengo wa kupotosha na kupandikiza chuki. Ukweli wa jambo hili ni kwamba, mwandishi huyo alivuka mipaka ya sheria za kupata habari kwakujaribu kulazimisha kwenda kuwarekodi wasanii Diamond na Zuchu katika eneo la hoteli ambalo waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia bali kwa wakazi wa hoteli hiyo pekee. Mlinzi tajwa na wenzie walitumia njia zinazoheshimu na kulinda haki za waandishi wa habari katika kumzuia.

Hata video inayosambazwa haioneshi mwandishi huyo akishambuliwa, baii inaonesha tu akizuiliwa na kisha video kukatishwa na kuonekana yuko chini. Kutokana na wingi wa waandishi wa Habari waliokuwepo, tunaamini isingekosekana video inayoonesha mwandishi huyo akishambuliwa. Kwa jinsi tukio hili linavyosambazwa na kuongelewa inatupelekea kuamini kwamba kuna viashiria vya kutaka kumchafua Mkurugenzi na Msanii wa lebo ya Wasafi.

Menejimenti ingependa kuwataarifu ya kuwa licha ya Diamond Platnumz kuwa Mwanamuziki lakini pia ni

muwekezaji mkubwa katika sekta ya habari. Na amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na wadau wote wa habari nchini. Hivyo si yeye tu bali hata wasaidizi na safu yake nzima inatambua, inaheshimu na kulinda haki za waandishi wa habari.

Tunatoa wito kwa vyombo vya habari kufuata mipaka ya kazi na sheria zilizotungwa katika kuheshimu utu, haki za faragha na ubinadamu. Pia kuepuka kutengeneza habari za uongo ambazo zinaweza kuleta chuki na kudhuru sifa, heshima ya tasnia na wanahabari wenyewe.

Pia, menejimenti ingependa kuwashukuru waandishi wote walioshiriki katika kufanikisha tamasha la msanii Zuchu iliyofanyika katika fukwe za Kendwa Rocks Kisiwani Zanzibar tarehe 24.02.2024. Lebo ya WCB Wasafi inathamini mchango wa waandishi wa habari na itaendelea kufanya kazi na

waandishi wa habari wote kwa ukaribu na kwa manufaa ya pande zote. Tunashukuru kwa uelewa wenu na tunawaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.

Imetolewa na:

UONGOZI WA LEBO YA WCB WASAFI".

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page