top of page

WAZIRI MKUU WA PAKISTAN AANZA ZIARA YA SIKU MBILI AZERBAIJAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI

Na Ester Madeghe,


Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif ameanza ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini Azerbaijan leo Jumatatu. Sharif ametua katika mji mkuu wa Baku jana Jumapili jioni akifuatana na ujumbe wa ngazi ya juu akiwemo Naibu Waziri Mkuu, Mohammad Ishaq Dar na wajumbe wengine wakuu wa Baraza la Mawaziri.


Hii ni ziara ya pili ya Sharif nchini Azerbaijan tangu kushika wadhifa huo Machi 2024. Sharif pia ameratibiwa kuhudhuria kongamano la biashara lililoandaliwa kwa ushirikiano na wakala wa kukuza Usafirishaji na Uwekezaji wa Jamhuri ya Azabajani.


Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan Pande hizo mbili zitashiriki katika majadiliano mapana kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, hususan katika sekta ya nishati, biashara, ulinzi, elimu na hali ya hewa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page