top of page

WAZIRI AWESO ATAKA SULUHISHO LA MAJI LIPATIKANE JIJINI DODOMA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka wataalamu kufanya uchunguzi wa kina juu ya swala la upatikanaji wa maji jijini Dodoma ili kuruhusu uchimbaji wa visima virefu katika mkoa huo Aweso ameyasema hayo akiwa katika ziara yake kwenye maeneo ya Miganga-Mkonze na Nkuhungu kuangalia hali ya upatikanaji maji jijini humo


“Rais Dk Samia Suluhu Hassan ametupatia vifaa vya kisasa vya utafiti wa kina wa upatikanaji wa maji hivyo vianze kazi hapa Dodoma mara moja ili kuendeleza hatua za uchimbaji wa visima virefu kutatua adha ya upatikanaji wa maji”


Ameongeza kuwa wakati wakiendelea kusubiri mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria na mradi wa bwawa la Farkwa aliwataka watendaji wa maji waendelee kuchimba visima maeneo tofauti ili kupunguza adha ya maji ndani ya mkoa huo


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma(DUWASA) Mhandisi Aron Joseph amesema mahitaji ya maji jijini Dodoma kwa siku ni lita milioni 147 na huku uzalishaji wa maji ni lita milioni 79 na hivyo kuwa na upungufu wa lita milioni 68 kwa usiku hali inayopelekea mgao mkubwa wa maji.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page