top of page

WATU WATATU WALIOTEKWA KWA MAANDAMANO YA GEN-Z KENYA WACHIWA

NA VENANCE JOHN


Raia watatu waliotekwa wakati wa maandamano ya vijana, nchini Kenya, maarufu kama maandamano ya Gen-Z wameachiliwa huru. Mashirika ya haki za binadamu nchini humo yamevishutumu vikosi vya usalama kwa kutotoa taarifa ya eneo walikokuwa wameshikiliwa.


Watu hao, waliofahamika kama Bob Njagi, Aslam Longton na kaka yake Jamil Longton, wanadaiwa kutekwa, Agosti 19 na wanaume waliojitambulisha kuwa maafisa wa polisi katika eneo la Kitengela, karibu kilomita 30 kusini mwa mji mkuu wa Nairobi.


Hivi karibuni, tukio hilo lilipamba moto baada ya mahakama mjini Nairobi kumtia hatiani naibu mkuu wa jeshi la polisi, Gilbert Masengeli, kwa kosa la kudharau mahakama, kutokana na kushindwa kutokea mahakamani ili kujibu maswali juu ya kutoweka kwa watu hao watatu.


Mamlaka Huru ya Usimamizi wa Polisi (IPOA) imesema inachunguza malalamiko kadhaa ya ukamataji wa kinyume cha sheria na utekaji kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali yaliozuka nchini Kenya mwezi Juni.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page