Na Ramla Ramadhan
Takribani watu 10 wamefariki dunia baada ya kutokea kwa mlipuko wa volkeno mashariki mwa Indonesia Mlipuko huo umetokea katika Mlima Lewotobi Laki-laki uliopo kwenye Kisiwa cha Flores katika jimbo la Nusa Tenggara Mashariki saa 23:57 kwa majira ya huko

Kulingana na Kituo cha Kukabiliana na Volkeno na Maafa ya Kijiolojia Indonesia imesema kuwa lava na mawe ya moto yaliruka hadi katika vijiji vilivyo umbali wa kilomita 4 kutoka kwenye volkeno na kuteketeza na kuharibu vijiji saba na maeneo ya wakazi hao.
Comments