Na VENANCE JOHN
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema mpaka sasa tayari wanawake 23 wamefanyiwa huduma ya upasuaji wa kubadili maumbile kwa kuboresha maumbile, upasuaji aliyouita ni upasuaji wa urembo kwenye hospitali hiyo tawi la Mloganzila.

Profesa Janabi amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya hospitali hiyo Upanga. Amesema upasuaji mwingine uliofanyika ni wa kuweka puto tumboni kwa watu 200 na wale wa kupunguza tumbo wakifikia 11,000.
“Mloganzila inaendelea na upasuji mbalimbali, ukiwemo wa masuala ya urembo na mambo mengine kwa mafanikio makubwa,” amesema Profesa Janabi. Amesema upasuaji mwingine uliofanyika Mloganzila ni kuwawekea magoti bandia wagonjwa 205 na upasuaji wa matundu madogo 12.
Comments