Na VENANCE JOHN
Orodha ya washindani wa mgombea mwenza wa Kamala Harris ndani ya chama cha Democrats inazidi kupungua baada ya waliotarajiwa kuwa washindani wa kusaka kuteuliwa na Kamala Harris kuendelea kung'atuka hivyo kuashiria kuwa Kamala Harris anaweza kuwa na machaguo machache ya kumpata mgombea mwenza.

Hii inakuja baada ya gavana wa jimbo la North Carolina, Roy Cooper na gavana wa jimbo la Michigan, Gretchen Whitmer kujiondoa kwenye harakati za kutafuta kuteuliwa na chama chao mgombea mwenza wa urais.
Hata hivyo inatarajiwa kuwa ikiwa Kamala Harris atachaguliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama chake, ili kuleta uwiano sawa na kuwashawishi wapiga kura, atalazimika kumteua mgombea mwenza ambaye ni mzungu ambaye wajuzi wa siasa za marekani wanasema atalazimika kuwa wa jinsi ya kiume.
Katika taarifa yake Roy Cooper hapo jana alisema "nilipewa heshima ya kufikiriwa kuwa mgombea mwenza. Huu haukuwa muda sahihi kwa North Carolina na kwangu hasa kwa nafasi hii ya kitaifa"
Naye Gretchen Whitmer akiwa kituo cha runinga cha CBS alisema hakuwa sehemu ya walengwa katika mchakato wa kumsaka mgombea mwenza wa Kamala Harris.
"Nimewasiliana na kila mtu, ikiwamo watu wa Michigan, kwamba naendelea kubaki kuwa gavana wa Michigan mpaka mwisho wa mhula wangu 2026", Whitmer amesema. Kamala Harris alipumzika kufanya kampeni mwisho mwa juma na kufanya mazungumzo ya faragha na baadhi ya watu anaofikiria kuwa wanaweza kuwa mgombea mwenza akiwamo gavana wa Pennsylvania, Josh Shampiro.
Wengine wanaofikriwa kuwa wanaweza kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kamala Harria ni gavana wa jimbo la Kentucky, Andy Beshear, seneta wa Arizona, Mark Kelly, gavana wa Minnesota, Tim Walz na waziri wa usafirishaji Pete Bttigieg
Comentarios