Na VENANCE JOHN
Wafanyabiashara wa soko kuu la Chifu Kingalu Mkoani Morogoro wamedaiwa kugoma kufungua biashara na kufunga barabara ya Madaraka wakishinikiza serikali kuwaondoa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa pembeni ya barabara.

Mwenyekiti wa soko hilo, Khalid Mkunyagela amedai kitendo cha wafanyabiasha wengine kuuza bidhaa nje ya maduka kinasababisha wateja kutoingia ndani ya eneo la soko kuu. Mkunyagela amesema hali hiyo inapelekea wafanyabiashara wa soko kuu kukosa wateja hivyo kupelekea kushindwa kulipa kodi ya pango.
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala akitolea ufafanuzi suala hilo amesema hakuruhusu wafanyabiashara wapange bidhaa pembeni ya barabara bali alitoa zuio wasipigwe na kumwagiwa vitu na watengewe eneo maalumu.
Comments