Na VENANCE JOHN
Klabu ya Ittihad Tanger inayoshiriki ligi kuu ya Morocco imesema kuwa msako unaendelea kuwatafuta wachezaji wawili waliotoweka katika Pwani ya Kaskazini mwa nchi hiyo katika

bahari ya Mediterani baada ya mikondo mikali ya bahari kutikisa boti waliyopanda.
Wachezaji hao walikuwa wamekodisha meli ya kifahari katika eneo la mapumziko la ufuo la M'diq - kaskazini mwa jiji la Tetouan, waliyokuwa wakisafiria.
Wahudumu watano wa Ligi Kuu ya Morocco ndio wanaoshiriki katika msako wa kuwasaka wachezaji hao.
Huduma za dharura ambazo ziliazimia kuwasaka wachezaji hao ziliwaokoa wachezaji 3 baada ya kisa hicho, lakini wachezaji Abdellatif Akhrif mwenye umri wa miaka 24, na Salman El-Harrak wa miaka 18, hawajapatikana mpaka sasa.
Wachezaji wengine Oussama Aflah, Soumaimane Dahdouh na Abdelhamid Maali, mchezaji wa kimataifa wa Morocco wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 20, waliokolewa baada ya kuwa baharini kwa saa kadhaa.
Rais wa timu ya Ittihad Tanger Bw. Mohamed Cherkaoui amethibitisha kuwa "utafutaji wa wachezaji waliopotea bado unaendelea".
Pia amewataka mabaharia na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii kuendelea kuwa makini na taarifa wanazotoa kuhusu wachezaji hao wawili ambao bado hawajapatikana.
Comentários