Na Kulwa Mwaijulu
Bunge la Serbia liliingia katika machafuko siku ya Jumanne wakati wabunge wa upinzani waliporusha maguruneti ya moshi na gesi ya kutoa machozi ndani ya chumba hicho kupinga serikali na kuunga mkono wanafunzi waliokuwa wakiandamana.

Huku makumi ya wabunge wakiwa wamekusanyika katika ukumbi huo, wabunge wa upinzani waliwasha moto na kurusha mabomu ya moshi na mayai, huku wengine wakirusha viti vyao na kusababisha moshi kujaa ndani ya jengo zima. Wanachama watatu wa chama tawala cha Serbian Progressive Party (SNS), akiwemo mwanamke mjamzito, walijeruhiwa katika vurugu hizo, huku mmoja akiugua kiharusi,
Machafuko hayo yanaashiria kuongezeka kwa kasi vuguvugu la maandamano linaloongozwa na wanafunzi ambalo limesababisha nchi kusimama, na kutoa tishio kali zaidi kwa utawala mkali wa Rais Aleksandr Vucic.
Mgogoro wa kisiasa wa Serbia ulianza baada ya mwavuli wa kituo cha gari moshi katika mji wa Novi Sad kuporomoka mwezi Novemba na kuua watu 15 hali iliyosababisha miezi minne ya maandamano ya karibu kila siku ambayo yamezua makundi makubwa ya jamii ya Waserbia na kufika kila kona ya taifa hilo la Balkan.
Mwavuli uliobomoka wengi wanaamini ulitokana na kazi mbovu na ya haraka iliyofanywa na wakandarasi wanyonge umekuja kutumika kama ishara ya kile ambacho wengi wanaona kama ufisadi katika taifa hilo.
Comments