top of page

WABUNGE KENYA WARIDHIA MJADALA WA KUMUONDOA MAKAMU RAIS RIGATHI GACHAGUA

Na VENANCE JOHN


Wabunge nchini Kenya wameridhia kuanza mjadala ili kumuondoa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kwa tuhuma kuwa amekuwa akikiuka sheria mbalimbali na katiba ya Kenya. Hatua hiyo ya kisiasa haijawahi kushuhudiwa kwa miaka yote ya uongozi nchini Kenya ambayo imekuwa ikijitanabaisha kuwa nchi ya demokrasia kwa ukanda wa Afrika Mashariki.


Naibu rais Gachagua anatuhumiwa kwa kuihujumu serikali, kuhusika katika ufisadi, ukaidi, kuendesha siasa za migawanyiko ya kikabila miongoni mwa mashitaka mengine kadhaa. Wabunge 291 walitia saini kuunga mkono hoja iliyowasilishwa bungeni, ikiwa ni zaidi ya idadi ya chini ya wabunge 117 inayotakiwa kuruhusu mjadala huo kuendelea.


Spika wa bunge la kitaifa, Moses Wetangula, amesema hoja hiyo iliyowasilishwa na Mutuse Eckomas Mwengi, mbunge kutoka muungano unaotawala, imefikia viwango vyote vya kikatiba vinavyohitajika.


Hoja hiyo inaorodhesha sababu 11 za kumshitaki Gachagua, ikiwa ni pamoja na kujikusanyia utajiri unaokadiriwa kuwa shilingi bilioni 5.2 katika kipindi cha miaka miwili dhidi ya mshahara wake wa jumla ya dola 93,000 kila mwaka. Mjadala na kura vinatarajiwa kufanyika Jumanne ya wiki ijayo kabla ya kupelekwa katika baraza la seneti.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page