top of page

URUSI YAISHAMBULIA UKRAINE KWA KOMBORA LA MASAFA MAREFU LA BALISTIKI BAADA YA UKRAINE KUTUMIA MAKOMBORA YA MAREKANI NA UINGEREZA

Na VENANCE JOHN


Urusi imerusha kombora la masafa marefu kutoka eneo la kusini mwa Astrakhan leo asubuhi kuishambulia Ukraine.

Makombora hayo yanaweza kusafiri maelfu ya kilomita na yanaweza kutumika kusambaza vichwa vya nyuklia, ingawa yanaweza pia kuwa na vichwa vya kawaida vya kivita. Jeshi la anga la Ukraine limesema, kwamba hiyo ni mara ya kwanza kwa Urusi kutumia kombora hilo lenye nguvu, la masafa marefu katika wakati wote wa vita.


Shambulio hilo linakuja baada ya Ukraine kutumia makombora ya Marekani na Uingereza kushambulia maeneo yaliyolenga shabaha ndani ya Urusi wiki hii, jambo ambalo Urusi ilikuwa imeonya kwa miezi kadhaa kwamba ingejibu shambulio la aina hiyo.


Jeshi la anga la Ukraine limesema, mashambulizi ya Urusi yalilenga makampuni na miundombinu muhimu katika mji wa Dnipro lakini hata hivyo haikuwa wazi kombora hilo la masafa marefu limelenga nini na iwapo lilisababisha uharibifu wowote au la.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page