Kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amepost picha hii kisha amefunguka haya
Utapeli wa aina 10 wa Viongozi wa KOLO kwa Mashabiki wao
1: Mimi nina uzoefu, Mkinichagua niwe kiongozi Yanga hawezi kutufunga, Viongozi wao vijana wale hawaniambii chochote. [ Sasa hivi ameanza kukimbia kuja uwanjani]
2: Kolo hafungwi na Yanga mvua ikiwa inayesha [5-1 ikazaliwa]
3:: Kolo akiweka kambi Zanzibar, Yanga hachomoki, Twendeni huko Tukajifungie [2-1 Swaafi wakachezea]
4: Kolo ikiunga nguvu na Friends Of Kolo washirikishwe, Yanga anakufa asubuhi tu [Vikao mpaka wametumia Calculator lakini wapi
5: Kolo ni kubwa sana, Haiwezi kufungwa mara mbili ndani ya Msimu mmoja [ Jumla ya Goli 7 zimepatikana Nje, Ndani]
6: Yanga hawezi kufikia mafanikio yetu Kimataifa, watatamba hapa hapa tu [Medali ya Shirikisho CAF iko Jangwani, Robo Fainali CAF CL
7: Sisi Kolo tuweke nguvu Kimataifa, Tutampasua Al Ahly na kumtoa [Wakaishia kutoa picha za Mayele tu
8: Kolo Tumeshusha mastraika wakuwatawanya bahari, watawafunga magoli ya kila aina. Ni funga funga hao [Derby wote wamekaa benchi wakikata kucha kwa meno
9: Aaah Kibu Dee ndio mechi zake, Diarra atakoma. Huyu ndio kiboko ya Yanga [Mechi 2 kwenye Derby hana On Target hata 1

10: Tumeiba kiungo wao Airport, huyu ni zaidi ya Aucho, Anajua sana, Ngojeni Derby ifike muone anavyobadilika na kuwa hatari [Alichoweza kubadili ni rangi ya Nywele Tu
Nb: Kwa sauti ya GSM "YANGA BINGWA" Ameandika Ally Kamwe.
コメント