top of page

Trump Asema Ukraine Imetuma Barua Kuomba Meza Ya Mazungumzo, Urusi Yataka Amani

Na VENANCE JOHN


Rais wa Marekani Donald Trump jana amesema amepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraini Volodymyr Zelenskiy ambapo kiongozi huyo wa Ukraine alionyesha nia ya kurudi kwenye meza ya mazungumzo kuhusu vita vya Urusi na Ukraine.


"Ukraine iko tayari kuja kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukreni," Trump alisema katika hotuba yake kwa Congress siku ya Jumanne wakati akinukuu barua hiyo. Trump pia alisema amekuwa kwenye majadiliano mazito na Urusi na kwamba amepokea ishara kwamba wako tayari kwa amani.


Trump alitarajiwa kueleza zaidi mipango yake kwa Ukraine na Urusi katika hotuba yake kwa Congress, lakini hakufichua maelezo zaidi kuhusu jinsi anavyopanga kumaliza mzozo mkubwa zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia. Trump alisema Ukraine iko tayari kutia saini mkataba wa madini na Marekani, ambao Washington inasema ni muhimu ili kupata uungwaji mkono wa Marekani kwa ulinzi wa Ukraine.


Trump hakutoa maelezo zaidi juu ya mpango huo wa madini, na hivyo kuacha wazi hatima yake. Mapema jana, Zelenskiy aliahidi kurekebisha uhusiano na Marekani baada ya kile alichoeleza kuwa mgongano uliotikea na Trump wiki iliyopita.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page