top of page

Trump Amtaka Zelensky Ikulu Ya Marekani Ijumaa Hii Kutia Saini Ya Mkataba Wa Madini

Na Kulwa Mwaijulu


Rais wa marekani Donald Trump amesema anatarajia kukutana na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky mjini Washington siku ya Ijumaa kutia saini mkataba wa madini baada ya afisa mkuu wa Ukraine kusema makubaliano ya kimkataba yamefikiwa.


Ripoti za vyombo vya habari zinasema toleo lililorekebishwa la waraka huo linaonekana kupunguza hitaji la Marekani la kupata dola za kimarekani bilioni 500 sawa na Tsh trilioni 130 kama mapato yanayoweza kupatikana kutokana na kupata madini ya Ukraine. Hata hivyo inasemekana hali hii haitoi hakikisho thabiti la kiusalama kwa Ukraine ambayo juzi (24/02/2024) ilitimiza miaka 3 katika vita na jirani yake Urusi.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page