Na Ester Madeghe
Manispaa ya Beit Lahiya kaskazini mwa Gaza imeutangaza mji uliokumbwa na maafa katika majuma kadhaa kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na jeshi la Israel. Wanajeshi wa Israel wamewauwa takribani Wapalestina 120 huko Beit Lahiya katika shambulio ambalo Marekani imeliita "la kuogofya".

Sam Rose, afisa wa UNRWA, amesema kuwa Israel imeinyima ruhusa UNRWA ya kuleta misaada kaskazini mwa Gaza isipokuwa katika hospitali kadhaa za kaskazini, ambazo zimekuwa zikivumilia kuzingirwa na jeshi. “Kwa kawaida hatupewi sababu, tunaambiwa kuwa haiwezekani kuwezesha ama kuwasaidia wahanga wa kiPalestina kwa sababu za kiutendaji," amesema afisa wa UNRWA
"Kazi nyingi za kutoa misaada zimefanikiwa katika baadhi ya maeneo ya mji wa Gaza, lakini hatujaweza kufika kaskazini mwa Mji wa Gaza, ambapo ndio kitovu cha wahanga wa mashambulizi ya Israel.
"Watu wanakufa kila leo, hali inayotuletea taswira mbaya, kwani mpaka sasa asilimia 10 ya wakazi wa Gaza wameuawa au kujeruhiwa. jambo ambalo haliepukiki, na unahisi nini kingine kinaweza kutokea zaidi kama UNRWA itawekewa ukomo kwenye kutoa misaada.
Kuhusu marufuku ya Israeli dhidi ya UNRWA kutoa misaada Gaza, Rose amesema "hakuna shirika lingine duniani linaloweza kuchukua na kubeba mzigo wa kuwasaidia wa Palestina, kama ambavyo UNRWA imekuwa ikifanya kwa takribani miaka 75 sasa.
Commentaires