top of page

TAKUKURU YABAINI UPIGAJI UNAOFANYWA NA ABIRIA TRENI YA MWENDO KASI (SGR)

Na VENANCE JOHN


Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Morogoro Bw. Christopher Mwakajinga amesema kuna changamoto ya baadhi ya abiria wa treni ya mwendo kasi (SGR) kusafiri umbali mrefu tofauti na gharama ya tiketi walizokata.


Mwakajinga amesema jambo hilo limepelekea Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuweka ukaguzi wa tiketi ili kudhibiti wanaofanya vitendo hivyo.


Mwakajinga amesema hayo leo Agosti 15, 2024 na kutoa rai kwa abiria kuwa waaminifu ili kuwezesha TRC kuendelea kutoa huduma zenye ubora. Baadhi ya wadau wamekuwa wakidai kuwa baadhi ya wahudumu wa SGR hununua tiketi kwa bei halisi kisha kuziuza kwa bei ya juu kwa abiria wanaokosa tiketi.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page