top of page

TABORA KINARA WASIYOJUA KUSOMA NA KUANDIKA, MATUMIZI MABAYA YA MAJI NA KUTOKUWA NA VYOO BORA

Na VENANCE JOHN


Imeelezwa asilimia 32 ya wakazi wa mkoa wa Tabora hawajui kusoma na kuandika, hivyo kuwa mkoa ambao ni kinara kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wa aina hiyo


Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojua kusoma na kuandika, kwani mkoa huo una asilimia 2.5 pekee ya watu wasiojua kusoma na kuandika.


Hayo yameelezwa na mtakwimu mwandamizi Mdoka Omary kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwenye kikao cha usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kilichofanyika Nzega, mkoani Tabora. Dar es salaam una asilimia 97.5 ya watu wanaojua kusoma na kuandika, huku Mkoa wa Tabora ukiwa wa mwisho kwa kuwa na asilimia 68.0 ya watu wanaojua kusoma na kuandika.


Hii ni kutokana na takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, ambapo pia mkoa wa Tabora umekuwa ukifanya vibaya kwa watu wake kutokuwa na vyoo bora na unashika nafasi ya tatu kutoka mwisho ukiwa na asilimia 33.8 huku mkoa wa mwisho ukiwa ni Kagera ambao una asilimia 32.2. Mtakwimu, Mdoka Omary amesema mkoa huo pia umetajwa kama mkoa unaofanya vibaya hata kwenye matumizi ya maji safi na salama kutoka kwenye vyanzo vilivyothibitishwa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page