Ofisa tabibu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Geita, Fimbo Ncheye (25) amedaiwa kujiua akiwa ndani ya chumba alichokuwa amelala huku akiacha ujumbe wa kuwaomba radhi wazazi wake kwa hatua alizochukua na kutaka mtu yeyote asilaumiwe juu ya kifo chake.
Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Thomas Mafuru amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema Ofisa Tabibu huyo alikua akijitolea kwenye kitengo cha wagonjwa wa nje (OPD) na

hakua mgonjwa na hakuwahi kueleza kama anatatizo lolote.
Dk Mafuru amesema hadi sasa hawajafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo na kwamba wanasubiri taratibu za kipolisi pamoja na familia ili mwili wake ufanyiwe uchunguzi.
Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa nyumba aliyofia Fimbo, Proses Mwiseo amesema usiku wa saa tano aligongewa na wapangaji wakidai wanasikia kelele za fujo kama mtu anaugulia na kuomba msaada lakini walipofika walikuta kelele zimetulia na walipogonga hakufungua mlango.
"Fimbo hakuwa anaishi hapa aliletwa na mwenye chumba ambaye ni rafiki yake na ana siku mbili hapa na ndani tumekuta ujumbe akiwaomba radhi wazazi wake kwa tukio alilofanya na kutaka asichukuliwe sheria mtu yoyote ni maamuzi yake binafsi"
Kwa upande wake Marco Madoshi Balozi Shina namba tatu katika mtaa wa Lwenge Kata ya Kalangalala amesema baada ya kutoa taarifa polisi walifika na kuvunja mlango na kumkuta kijana huyo yuko kwenye uvungu wa kitanda na ndani ya chumba kulikuwa na dawa zilizopondwa pamoja na dawa ya hospitali pamoja na sindano ambayo haijatumika.
Comments