Na VENANCE JOHN

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema tangu treni ya kisasa inayotumia umeme ya SGR kuanza kutoa huduma ya usafirishaji, tayari imekusanya kiasi cha Tsh bilioni 15.69. Ikumbukwe SGR ilianza kutoa huduma mwezi Juni tarehe 14, 2024 na kufikia Septemba 3, 2024, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limefanikiwa kukusanya kiasi hicho.
Prof. Mbarawa amesema kwa kipindi hicho, SGR imesafirisha Abiria 645,421 katika safari zake za kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro na Dar es Salaam kwenda Dodoma. Takwimu hizi ni za miezi 3 tu, kwani ni kutokea mwezi Juni mpaka Septemba mwaka huu 2024.
Comments