top of page

RASMI KENYA YAWASILISHA HATI ZA RAILA ODINGA KUGOMBEA UENYEKITI WA TUME YA UMOJA WA AFRIKA

Na VENANCE JOHN


Serikali ya Kenya imewasilisha rasmi nyaraka za kumuunga mkono mgombea wake, Raila Odinga, katika azma yake ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC). Wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya kigeni Korir Sing'oei, wajumbe wa Kenya waliwasilisha hati hizo kwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dharmraj Busgeeth na kwa Ofisi ya Wakili wa Kisheria wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa cnhin Ethiopia.





Kulingana na Sing'oei, vipaumbele vya Raila katika usukani wa umoja wa Afrika vitajumuisha; Ushirikiano wa Afrika na Maendeleo ya Miundombinu, Mabadiliko ya Kiuchumi, Kuimarisha Biashara ya Ndani ya Afrika, Uhuru wa Kifedha, Usawa wa Jinsia , Mageuzi katika kilimo, Hali ya Hewa, Amani na Usalama na Ajenda ya kuwazesha vijana Afrika.


Ikumbukwe kuwa miezi ya karibuni baada ya Raila Odinga kuonesha nia yake ya kusaka cheo hicho ndani ya umoja wa Afrika, serikali ya nchini Kenya chini ya Rais Wiliam Ruto ilisema itamuunga mkono, jambo lililowashangaza wengi kwani Raila Odinga ni mpinzani wa serikali iliyopo madarakani na aliwahi kuhamasisha maandamano dhidi ya serikali mwaka jana.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page