top of page

Rais Wa Korea Kaskazini Aamuru Jeshi Kuandaa Silaha Za Nyuklia

Na Ester Madeghe,


Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameamuru matayarisho kamili ya mashambulizi ya nyuklia, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kushuhudia jaribio la makombora ya masafa marefu.


Kwa mujibu wa shirika la habari la nchi hiyo (KCNA), jaribio hilo la silaha limeazimia kuwaonya wale wanaowaita maadui wanaoingilia mazingira ya kiusalama ya nchi hiyo. Shirika hilo limemnukuu Kim akisema ni jukumu la kikosi cha nyuklia kwenye jeshi la nchi yake kuwa tayari wakati wowote kuilinda Korea.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka wizara ya ulinzi ya Korea Kusini, jeshi la Korea Kaskazini limefanya majaribio yake ya makombora yanayosafiri kwa kasi baharini siku ya Jumatano. Aina hiyo ya makombora haimo kwenye orodha ya yale yaliyopigwa marufuku na Umoja wa Mataifa, ingawa yanaweza kubeba vichwa vya nyuklia.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page