
PROF. JANABI AWEKA WAZI MARA YA MWISHO KUNYWA JUICE NI MIAKA 24 ILIYOPITA "OGOPA VITU VITAMU TAMU"
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema utumiaji wa sukari kupita kiasi haufai kwa afya ya mwanadamu ambapo amesema mara ya mwisho yeye kunywa Juice ni mwaka 2000 sawa na miaka 24 iliyopita.
"Ukinywa glass moja asubuhi machungwa matano, mchana matano na jioni matano maana yake kwa mwezi ni machungwa 450, unaharibu afya yako, ogopa zaidi vitu vitamu tamu, unavyozungumzia sukari sio sukari tu bali ni vitu vitamutamu. Pale Muhimbili tunao watoto wa miaka tisa wana kisukari." amesema Profesa Janabi
Amasema hayo mkoani Mwanza wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Mafunzo wa 108 wa watayarishaji wa vipindi vya Elimu kwa Umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Washiriki wa mkutano huo ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali
Comments