top of page

POLISI YAMKAMATA MISS RWANDA 2022 KWA KUENDESHA GARI HUKU AKIWA AMELEWA

Kutoka nchini Rwanda, Jeshi la imetangaza kumkamata Mshindi wa Miss Rwanda 2022 Divine Muheto kwa tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa kitu ambacho adhabu yake ni faini ya Laki Moja na nusu pesa ya Rwanda na kufungwa Gerezani kwa siku tano.


Katika tangazo hilo linasema kuwa Miss Divine Muheto alikuwa anaendesha gari kinyume na sheria kutokana na kutokuwa na leseni ya udereva na kutoroka eneo la ajali baada ya kugonga miundombinu, polisi walisema Muheto hadi kufikia sasa hajazungumzo kitu chochote kuhusiana na shutuma hizo.


Muheto mwenye umri wa miaka 21 alifahamika mwaka wa 2022 baada ya kubeba taji la Miss Rwanda kabla ya Serikali ya Rwanda kuyapiga marufuku mashindano hayo kwa madai ya kuwepo kwa shutuma za unyanyasaji na utovu wa maadili kutoka kwa waandaaji. Kukamatwa kwa Divine Muheto kumekuja baada ya hivi karibuni mlimbwende huyo kuripotiwa kupata ajali akiwa amelewa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page