Na VENANCE JOHN
Polisi nchini Israel wamemkamata msaidizi mkuu wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu kwa madai ya kuvujisha taarifa za siri kwa vyombo vya habari vya kigeni. Viongozi wa upinzani wanasema taarifa za kijasusi zilighushiwa, na sehemu ya njama ya kuzuia makubaliano ya kusitisha mapigano na utekaji nyara huko Gaza.

Uchunguzi huo unahusu madai kwamba ofisi ya waziri mkuu ilitoa kipaumbele kwa vyombo vya habari vya kigeni kwa madai kwamba HAMAS inapanga kuwasafirisha mateka nje ya Gaza kwenye mpaka wa Misri na kuleta mgawanyiko katika jamii ya Israel ili kumshinikiza Netanyahu kuachilia huru mateka na makubaliano ya kusitisha mapigano.
Eliezer Feldstein, ambaye ametajwa na wanasiasa wa upinzani kama msaidizi wa Netanyahu, ni miongoni mwa watu kadhaa wanaohojiwa kuhusu uvujaji wa taarifa za siri na taarifa nyeti za kijasusi.
Amri ya mahakama iliyotangazwa kwa umma siku ya hapo jana ilisema kwamba taarifa zilizochukuliwa kutoka kwenye mifumo ya jeshi la Israel na zikutolewa kinyume cha sheria huenda ziliharibu uwezo wa Israel kuwakomboa mateka wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza.
Hata hivyo msemaji wa Netanyahu amekanusha kuwa kumekuwa na uvujaji kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu na kwamba mtu anayehusika hakuwahi kushiriki katika mijadala inayohusiana na usalama.
Kiongozi wa upinzani Yair Lapid jana aliishutumu ofisi ya waziri mkuu kwa kuvujisha nyaraka za siri ili kuzidisha uwezekano wa makubaliano ya kuchagiza oparesheni ya ushawishi wa maoni ya umma dhidi ya familia za mateka.
Comments