Peter Anthony Morgan, mwimbaji anayeongoza kundi la Morgan Heritage, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 47. Familia yake imetangaza kifo chake siku ya leo Jumapili ambapo Chanzo cha kifo chake hakikuwekwa wazi.
"Ni kwa upendo wa dhati kwamba tunawataarifu kwamba mpendwa wetu, baba, mwana, kaka na mwimbaji kiongozi wa Morgan Heritage Peter Anthony Morgan amepanda daraja leo Februari 25, 2024. Jah njoo utuokoe kutoka kwetu kwa sababu upendo ndio njia pekee. ," imeandikwa kwenye chapisho la taaifa ya msiba.
Na kumalizia
"Familia yetu inakushukuru mapema kwa upendo wako mwingi na msaada wako, na tunaomba maombi yako endelevu tunapopitia kipindi hiki. Tunakuomba uheshimu faragha yetu wakati huu."

Comments