top of page

PAPA FRANCIS AWATAKA WAUMINI KUFUNGA NA KUIOMBEA AMANI DUNIA

Na VENANCE JOHN


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewataka waumini wote kufunga na kuombea amani ya ulimwengu, wakati dunia ikikumbuka mwaka mmoja toka kuanza kwa mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza.


“Kadri pepo za vita na machafuko zinavyoendelea kuiharibu dunia na mataifa mengine, jumuiya ya Wakristo inakumbushwa kusali na kutafakari amani ya dunia,” Papa Francis amesema. Kulingana na Papa Francis, mgogoro huo, sio tu kwamba umeleta maafa ya kibinadamu, lakini pia umechochea mabadiliko tofauti ya kisiasa ulimwenguni.


Mashambulizi, yaliyodumu kwa mwaka mmoja sasa, yameua watu takribani 41,900, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine zaidi ya 97,000, kulingana na mamlaka za afya za Gaza.


Israeli pia inakabiliwa na kesi ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kufuatia vitendo vyake dhidi ya Gaza, mashtaka ambayo hata hivyo yana kanushwa vikali na mamlaka za Israel.

Komentáře


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page