Na VENANCE JOHN
Papa Francis ametembelea vijiji vya ndani ya msitu wa taifa la kisiwa cha Papua New Guinea leo Jumapili kuwatembelea Wakatoliki wanaoishi katika moja wapo ya maeneo ya mbali zaidi na kupeleka vifaa vya matibabu na misaada mingine.

Papa Francis amesafiri na kikundi kidogo cha wasaidizi wake kwenda katika kijiji cha Vanimo, kitongoji cha watu wapatao 12,000 kwenye kona ya kaskazini-magharibi ya kisiwa kikuu cha Papua New Guinea, kijiji ambacho hakina maji ya bomba na chenye uhaba wa umeme.
Papa Francis amepeleka mamia ya kilo za bidhaa kusaidia wakazi wa eneo hilo, ikijumuisha dawa, nguo mbalimbali, pamoja na vinyago na vyombo vya muziki vya watoto wa shule. “Mnaishi katika nchi yenye fahari, iliyotajirishwa na aina mbalimbali za mimea na ndege,” Papa Francis amewaambia wanakijiji cha Vanimo.
Papa amewataka wakatoliki wa eneo hilo kufanya kazi ya kukomesha tabia mbaya kama vile vurugu, ukafiri, unyonyaji, matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya, maovu ambayo amesema yanafunga na kuondoa furaha kwa ndugu wengi.
Comments