Na Ester Madeghe,

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amelaani vuguvugu la Wapalestina baada ya jeshi la Israel kusema kuwa moja ya miili iliyotolewa na Hamas haikuwa ya mateka yoyote wanaoshikiliwa huko Gaza, na kuituhumu kukataa kusitisha mapigano. "Huu ni ukatili mkubwa na wa kinyama Hamas wameufanya, ambao umevuka mipaka," alisema katika taarifa ya video.
Netanyahu ameongeza kuwa serikali yake "itahakikisha Hamas inalipa gharama kamili kwa ukiukaji huu wa kikatili na mbaya wa makubaliano". Waziri Mkuu huyo, ameahidi kwamba atafanya kazi kuwarudisha nyumbani "mateka wetu wote - walio hai na waliokufa".
Comments