Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya ,"Nimewatazama Wapinzani wote msimu huu naiona Simba yetu ikifanya maajabu ya dunia

Mpaka sasa Simba ndio timu yenye Wachezaji bora wenye viwango vikubwa mno, kilichobaki ni Mwalimu kutengeneza timu yenye mtiririko, muunganiko na maelewano ya pamoja. Eneo pekee linalohitaji nguvu mpya ya Nje ni eneo la Ushambuliaji nalo viongozi wetu wanakamilisha mpango hivi punde
Wana Simba tuwe na subira tumpe nafasi Mwalimu wa kufanya kazi yake tutakapoanza kula matunda ya furaha kila mtu atapata tunda lake. Ubaya Ubwela unaenda kukamilika" Ameandika Ahmed Ally.
Comments