Mfichuzi wa sakata la mpango wa kampuni ya Adan ya nchini India kutaka kukodishwa uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya wa Jomo Kenyatta (JKIA), Bw. Nelson Amenya, amesema anahofia uhai wake na kwamba maisha yake yako hatarini.

Wiki iliyopita, Waziri wa Fedha nchini Kenya, John Mbadi alikiri kwamba alishtushwa baada ya kugundua kwamba Mamlaka ya Usimamizi wa Uwanja wa Ndege ya Kenya (KAA) ilichukua siku moja tu kuidhinisha pendekezo la kampuni ya Adani mwezi Machi 2024. Nelson Amenya amesema alifichua mpango huo kwa sababu kwa sasa yuko nchini Ufaransa masomoni, lakini anaweza kulengwa na mahasimu wake hata akiwa nje ya Kenya.
Ufichuzi wa Amenya ulichochea hasira nchini Kenya na kusababisha mgomo mkubwa uliofanywa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta pamoja na kuanzishwa uchunguzi kamili bungeni kuhusu mpango huo.
Comments