Na VENACE JOHN
Baba wa mwanafunzi Mfaransa pamoja wa wanaume wengine 4 ambao walihusika kumuua mwalimu wa sekondari ambae alitumia katuni kuonesha taswira ya Mtume Muhammad. Kisa hicho kilisababisha mauaji ya kikatili ya mwalimu huyo. Leo watuhumiwa wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kujihusisha na mtandao wa kigaidi.

Mwaka 2020 siku chache tu baada ya Samuel Paty kuwaonyesha wanafunzi wake michoro ya katuni zinazomwonesha Mutume Mohammad, mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18 mwenye asili ya Chechnya, Urusi alimdunga kisu kwa kurudia rudia na kumuua nje ya shule yake huko Conflans-Sainte-Honorine karibu na Paris. Samuel aliuawa akiwa na miaka 47 mwaka 2020,
Hayo yamejiri baada ya babake Brahim Chnina kuchapisha mfululizo wa video kwenye mitandao ya kijamii akimtuhumu Samuel Paty kwa kumwadhibu bintiye kwa kulalamika darasani, akitaja jina la Samuel Paty na kuitambulisha shule.
Waendesha mashtaka wanamshutumu Chnina kwa kushirikiana na Abdelhakim Sefrioui, ambaye alianzisha shirika lenye msimamo mkali wa Kiislamu, ili kuchochea chuki dhidi ya mwalimu huyo wa shule ya sekondari. Waislamu wengi wanaona taswira yoyote ya Mtume Mohammad kuwa ni kufuru.
Comments