MZUNGU HAACHWI KIRAHISI KUMBE DADA ALIFANYA KIKI...
Siku chache zilizopita tulikujuza kuhusiana na uvumi wa kuachana kwa mwanamitandao wa Kenya maarufu kama Vanny mwenye umri wa miaka 23 na mume wake wa miaka 63, lakini mwanadada huyo amekuja kubadilisha maneno yake huku mambo yakionekana kuzidi kunoga na kusherehekea siku yao ya 3 ya mahusiano kuvuma kuwa wametengana tangu kutangaza

talaka yao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanadada huyo ameandika maneno yenye kumaanisha kwamba, "Wacha tuweke hili sawa, uvumi unaoenea juu yangu na Brad kuachana sio kweli
Tunafurahi kuona wale wote ambao walikuwa wakingojea anguko letu na wale ambao tunawatia moyo na wanapenda sana uhusiano wetu. Asante kwa kila mtu anayetuunga mkono na sote tutasherehekea siku hii. Furaha ya kumbukumbu kwetu. Ni mimi Umpendae, VannyandBrad. Milele pamoja hapa hataachwa mtu!"
Comments