top of page

MZAZI WA MWANAFUNZI ALIYEWAUWA WENZAKE GEORGIA, MAREKANI AKAMATWA NA KUSHTAKIWA

Na VENANCE JOHN


Mamlaka katika jimbo la Georgia nchini Marekani wamemkamata Baba mzazi wa mtoto wa miaka 14 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili ya juu (high school), aliyewaua wenzake 2 na walimu 2 na kuwajeruhi wengine 9.


Mwanafunzi kwa jila la Colt Gray ambaye anasoma shule ya Apalachee, eneo la Winder, Georgia ameshitakiwa kwa makosa ambayo ni kuua bila kukusudia, makosa mawili ya mauaji ya daraja la pili, na makosa nane ya ukatili kwa watoto.


Babaye Colt Gray ambaye kwa sasa ana miaka 54 amekamatwa na kujumuishwa kwenye kesi ya mwanae. Colin Gray ambaye ni baba wa Colt Gray anashitakiwa kwa kuwa akiwa anajua alimruhusu mwanaye kumliki bunduki.


Colin Gray alimnunulia bunduki mwanae Colt Gray kama zawadi mwezi Disemba mwaka 2023 na ndiyo iliyotumiwa na mwanae kuwaua wanafunzi wenzake 2 na walmu 2 huku wengine 9 wakijeruhiwa.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page