Na VENANCE JOHN
Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine msanii ambaye pia ni mwanasiasa kijana amepigwa risasi na polisi baada yakutokea mvutano baina yake na polisi.

Msanii huyo ambaye ni kiongozi wa chama cha NUP amepigwa risasi kwenye mguu akiwa katika hali ya mvutano na polisi katika kijiji cha Bulindo nchini humo. Kiongozi juyo amekimbizwa hosipitali kwa ajili ya matibabu.
Mtu anayesimamia ukurasa wa mtandao wa X (twitter) wa Bobi Wine ndiye aliyetoa taarifa za mwanasiasa huyo kupigwa risasi ya mguu. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na polisi kuhusu tukio hilo.
Comentários