top of page

MWANAMKE APIGANIA UHAI WAKESAA 2 BAADA YA CHATU KUMNASANA KUJIVILINGISHA MWILINI MWAKE.


Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni unaambiwa Mwanamke nchini Thailand amenusurika kupoteza uhai baada ya kutumia saa mbili kupigania maisha yake huku chatu mwenye urefu wa mita nne akiwa amejiviringisha mwilini kwake. Arom Arunroj alikuwa akiosha vyombo nyumbani kwake mji wa Samut Prakan alipohisi kitu kikimuuma mguuni.


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 64 awali alidhani aling'atwa na mjusi, kabla ya kugundua kuwa ni chatu. Jitihada zake za kujilinda dhidi ya nyoka huyo mwenye uzito wa kilo 20 hazikufaulu, na kumuangusha chini. Arom alipambana kujitoa kwa chatu huyo huku akiomba msaada.


Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page