top of page

Mwanamke Aliyembusu Msanii Wa Kiume Shingoni Asakwa Na Polisi, Wasema Amenyanyasa Msanii

Na Ester Madeghe,


Mwanamke wa Kijapani ambaye bila kutarajia alimbusu msanii kwa jina la Jin wa bendi ya K-pop katika hafla ya mashabiki mwaka jana amejikuta akichunguzwa na polisi wa Korea Kusini.


Polisi wa Korea Kusini wametoa wito kwa mwanamke huyo, kujitokeza kuhojiwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia katika eneo la umma. Baada ya kumkumbatia nyota huyo, mwanamke huyo alionekana kumbusu uso wake, huku Jin akijibu kwa kugeuza uso wake pembeni.


Busu hilo liliwakasirisha mashabiki wengine, ambao mmoja wao aliwasilisha malalamiko ya uhalifu dhidi yake, na kusababisha polisi kuanzisha uchunguzi. Wakati wa utumbuizaji wake uliodumu kwa saa tatu, mashabiki walimkumbatia msanii huyo mwenye umri wa miaka 33, lakini mmoja wao alizua ghasia alipoonekana kubusu uso wa Jin.


Video za tukio hilo zilisambaa mitandaoni kwa haraka, kwamba Jin pia, alishangazwa na hatua hiyo, ambapo Jin, alijaribu kugeuza kichwa chake huku akimkumbatia mwanamke huyo kabla ya kwenda kwa shabiki mwingine haraka. Utambulisho wa mwanamke huyo haujatambulika bado, lakini polisi waliongeza kuwa wamemtambua kwa usaidizi kutoka kwa wenzao wa Japan.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page