top of page

MWANADADA WA NIGERIA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUCHOMA KISU MUMEWE HADI KUFARIKI KISA PESA ZA WALIZOTAPELI MTANDAONI......

Maafisa wa polisi kutoka Jimbo la Imo Nchini Nigeria, wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 27 aliyetambulika kwa jina la Oluchi Nzemechi kwa tuhuma za kumdunga kisu



mume wake Kelechi Nzemechi hadi kufariki kutokana na kutofautiana kuhusu utaratibu wa kugawana mapato yatokanayo na utapeli wa mtandaoni huku tukio hilo likiripotiwa kutokea Juni 2 mwaka huu.

Taarifa kutoka kwenye vyombo vya usalama wa jimbo hilo inasema, wakati wa kuhojiwa mshukiwa alisimulia jinsi marehemu alivyomshawishi katika uhalifu wa mtandao.

Alisema walifanikiwa kumlaghai raia wa Indonesia Rupiah milioni 250 lakini kukataa kwake kumpa sehemu yake ya fedha hizo kulisababisha ugomvi na katika mchakato huo, alimchoma kwa kisu cha jikoni.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, mtuhumiwa huyo alisema alipogundua kuwa amefariki, alichukua karatasi na kuandika, “Unadhani unaweza kula pesa zangu na kwenda bure? Mimi ni baba kwa wavulana. Ninakuja kwa ajili ya mke wako na mtoto wako, ikiwa ni pamoja na familia yako,” na kuiweka juu ya maiti ya mwathiriwa kabla ya kutoroka nyumbani huku lengo lake likiwa ni kukwepa ushahidi wa kile alichofanya kujiokoa kwenye mikono ya sheria lakini bado amekamatika na taratibu nyingine za kimahakama zinaendelea.

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page