top of page

MwanaChuo Afariki Akisubiri Basi Stendi

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jordan mkoani Morogoro Magnos Mkinga (22) amefariki dunia katika stendi kuu ya mabasi ya Msamvu akidaiwa kuzidiwa ghafla na homa akiwa anasubiria usafiri wa kwenda Ruvuma.


Taarifa ya kifo hicho iliyotolewa leo Jumapili Machi 2, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, inaeleza: "Mtu aliyefahamika kwa jina la Magnos Simon Timoth Mkinga (22), mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Jordan, mwaka wa kwanza, mkazi wa Kipera, mkoani Morogoro alizidiwa ghafla na kujilaza chini mbele ya dada yake aitwaye Anna Osward Mbonde (42), mkazi wa Kibaha wakati wanasubiri usafiri wa basi la Kampuni ya Super Feo kwenda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili ya matibabu.


"Juhudi za kumfikisha hospitali zilifanywa na gari ya polisi iliyokuwa doria, lakini alipofikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ilibainika tayari alifariki dunia. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi, ndugu zake walikuwa katika mpango wa kutafuta matibabu zaidi ili kuimarisha afya yake."


Source: Mwananchi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page