Kamti ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 12, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo
Mechi Namba 201: Young Africans SC 1-0 Kagera Sugar FC Mwamuzi msaidizi namba mbili wa mchezo tajwa hapo juu, Shaban Mussa kutoka Geita ameondolewa kwenye ratiba ya

waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.
Mwamuzi huyo alikataa bao halali lililofungwa na mchezaji Joseph Guede wa klabu ya Yanga kwa tafsiri yake kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 42:1(1. ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ametozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kufanya vurugu ikiwemo kuwashambulia kwa maneno makali waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu.
Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Comments