top of page

MTOTO WA MIAKA 13 ASHITAKIWA KWA KUSHIRIKI MAANDAMANO YA VURUGU NCHINI UINGEREZA

Na VENANCE JOHN


Mtoto wa miaka 13 ambaye ni msichana, aliyekamatwa wakati wa kupambana na vurugu za maandamano leo amefikishwa mahakamani kusikiliza mashitaka yanayomkabili kwa kosa la kushiriki maandamano yaliyoanzishwa na watu wenye msimamo mkali wanaopinga wahamiaji na waislamu nchini Uingereza.





Mtoto huyo amekiri kosa la kukiuka sheria na kushiriki vurugu katika maandamano nje ya hotel iliyopo Aldershot Julai 31, hoteli ambayo inawahifadhi wahamiaji wanao tafuta hifadhi nchini Uingereza. Msichana huyo ni miongoni mwa watu wazima wengine wengi walioonekana mahakamani leo kujibu mashtaka yanayowakabili juu ya kuhusika kwao na vurugu.


Mpaka sasa watu wengine wengi ndani ya Uingereza wameshahukumiwa kwenda jela kwa kusababisha vurugu baada ya maandamano kuzuka yaliyotokana na taarifa potofu kuenea mtandaoni kuwa watoto waliochomwa visu na kuuawa, waliochomwa na mhamiaji ambaye alikuwa muislamu.


Mtoto huyo alihudhururia kwenye mahakama ya mkoa ya Basingstoke, ambayo kwa leo ililazimika kuketi kama mahakama ya watoto kwa ajili ya kusikiliza mtoto huyo aliyekuwa ametolewa ripoti yake toka awali.Mtoto huyo ameachiliwa kwa dhamana bila masharti baada ya kukiri kosa.


Amekiri kosa moja tu la kutumia au kuleta vurugu kinyume cha sheria. Hata hivyo hakuna taarifa za kina za ushahidi zilizotolewa. Kesi hiyo imesogezwa mbele mpaka Septemba 20, 2024 kwa ajili ya ripoti ya awali ya hukumu kutoka kwa mahakama hiyo ya watoto.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page